Venezuela yachagua rais na Cuba yatazama

Imebadilishwa: 6 Oktoba, 2012 - Saa 17:50 GMT

Wananchi wa Venezuela wanapiga kura kumchagua rais na uchaguzi huo unafuatiliwa kwa makini na watu wa Cuba kuona nani atashinda.

Wagombea urais wa Venezuela, Henrique Capriles na Hugo Chavez

Rais Hugo Chavez, msoshalisti, ana uhusiano wa karibu na Fidel Castro, na tangu Rais Chavez kuwa kiongozi wa Venezuela amezidisha ushirikiano na Cuba inayoongozwa na chama cha kikoministi - ushirikiano wa kisiasa na kiuchumi.

Cuba inanunua mapipa laki moja ya mafuta kutoka Venezuala kila siku kwa bei nafuu sana.

Mafuta hayo rahisi yameisaidia serikali ya kikoministi ya Cuba kuweza kuendelea.

Cuba nayo inatuma Venezuela madakatri, makocha wa michezo na walimu kuwasaidia wananchi maskini wa Venezuela.

Kisiasa nchi hizo mbili ni washirika wakubwa.

Lakini mgombea urais wa upinzani nchini Venezuela, Henrique Capriles, ameahidi kuwa akishinda ataacha kuisaidia Cuba na mafuta.

Wacuba hawakusahau kiza, shida na njaa ya miaka ya 1990, wakati msaada wa kiuchumi waliokuwa wakipata kutoka Umoja wa Sovieti uliposimamishwa baada ya umoja huo kuvunjika.

Wana-uchumi wa serikali wanasisitiza kuwa uchumi wa Cuba umebadilika sasa na sekta mpya zimechipuka, kama utalii kwa mfano.

Hata hivo, biashara na Venezuela ni thuluthi ya pato la kisiwa hicho.

Kwa hivo mbali ya siasa, wananchi wengi wa Cuba kwa sababu ya masilahi yao, watapenda Hugo Chavez ashinde katika uchaguzi wa leo

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.