Ufilipino yafikia mapatano na Waislamu

Imebadilishwa: 7 Oktoba, 2012 - Saa 10:10 GMT

Serikali ya Ufilipino imefikia makubaliano ya amani na kundi kubzwa kabisa nchini humo la wapiganaji wa Kiislamu, ili kumaliza mzozo uliouwa watu zaidi ya 120,000 katika miongo mine.

Rais Benigno Aquino wa Philippines

Makubalino hayo na kundi la Moro Islamic Liberation Front (MILF), yanakusudiwa kuanzisha eneo la Waislamu litalokuwa na madaraka ya kadiri fulani kusini mwa nchi, linaloitwa Bangsamoro.

MILF imesema imefurahi sana na Rais Benigno Aquino alisisitiza kuwa mpango huo unajumuisha makundi yote yaliyotaka kujitenga.

Lakini ukubwa wa eneo hilo jipya la Waislamu hujulikani, na lazima mpango huo ukubaliwe kwa kura ya maoni ya wananchi ambao wengi wao ni Wakatoliki.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.