Wapinga mtambo wa nuklia India

Imebadilishwa: 8 Oktoba, 2012 - Saa 15:03 GMT

Mamia ya watu nchini India wameandamana kupinga kile wanachosema ni serikali kuweka mafuta katika mtambo mpya tatanishi wa kawi ya nuklia.

Wameelezea wasiwasi kuhusu usalama katika mtambo huo mpya wa 'Kudankulam' ulioko katika jimbo la Tamil Nadu.

Mtambo huo upo katika eneo ambalo hukumbwa na mitetemeko ya mara kwa mara ya ardhi.

Serikali inasema kuwa mtambo huo umetimiza matakwa yote ya kiusalama kwa raia na utaweza kutumika kukidhidi mahitaji ya kawi nchini India.

Polisi na wanajeshi walizima maandamano hayo, yaliyoanzishwa hasa na wavuvi na wanavijiji waliokusanyika kwenye mitumbwi karibu na mtambo wenyewe

Mwezi jana mahakama ya juu ilitupilia mbali ombi la wanaharakati wanaopinga kawi ya nuklia kusitisha shughuili ya kuweka mafuta kwenye mtambo huo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.