Al Shabaab lapiga marufuku 'Islamic Relief'

Imebadilishwa: 8 Oktoba, 2012 - Saa 14:23 GMT

Mlinzi wa Al Shabaab akishika doria wakati chakula cha msaada kikitolea kwa wakimbizi

Wapiganaji wa kiisilamu wa kundi la Al Shabaab wamepiga marufuku shirika la mwisho la misaada lililosalia kufanya kazi katika maeneo wanayodhibiti.

Al-Shabaab imetuhumu shirika hilo la Uingereza, Islamic Relief, kwa kuendesha shughuli zake kwa niaba ya shirika la mpango wa chakula duniani WHO ambalo limepigwa marufuku katika maeneo hayo.

Islamic Relief limekanusha madai hayo na kuomba liruhusiwe kuendesha shughuli zake.

Shirika hilo linatoa chakula , maji na huduma za afya kwa zaidi ya watu milioni moja nchini Somalia.

Al Shabaab lingali linadhibiti maeneo ya vijijii na Kusini mwa Somalia licha ya kufurushwa kutoka miji mikubwa ya Somalia.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.