Wapiganaji Mali wanunua watoto jeshini

Imebadilishwa: 11 Oktoba, 2012 - Saa 08:05 GMT

Wapiganaji wa Tuareg

Wapiganaji wa kiisilamu wanaodhibiti sehemu za Kaskazini mwa Mali, wanajipatia pesa kutoka kwa biashara haramu ya mihadarati na kupitia kwa visa vya utekaji nyara ambapo wanalipwa kikombozi ili kuwaachilia mateka.

wakati wakitumia sheria ya kiisilamu katika maeneo wanayodhibiti.

Madai haya ni kwa mujibu wa afisaa mmoja mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Wapiganaji hao pia wananunua watoto kuwatumia kama wanajeshi, huku wakilipa familia za watoto hao dola mia sita kwa kila mtoto. Alisema Ivan Simonovic baada ya kuzuru nchi hiyo.

Wapiganaji hao wenye siasa kali, walitwaa thuluthi mbili za udhibiti wa Mali, wakati nchi hiyo ilipotumbukia katika vita baada ya kufanyika mapinduzi ya kijeshi.

Bwana Simonovic alitoa picha ya kutisha kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanyika katika eneo hilo.

''Haki za wanawake hasa zinakiukwa pakubwa'' alisema afisaa huyo ambaye ni naibu wa katibu mkuu kuhusu haki za binadamu katika Umoja wa mataifa ,akielezea kuhusu orodha ya wanawake ambao hawajaolewa au wale ambao walikuwa wamepata watoto.

Wanawake zaidi wanalazimishwa kuolewa huku gharama ya kupata mke ikiwa dola elfu moja.

''Visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu hapa ni vya kushtua na vinafanyika sana'' aliambia waandishi wa habari mjini New York, akiongeza kuwa wapiganaji hao wanatumia sheria kali za kiisilamu kudhibiti eneo hilo.

Katika ziara ya afisaa huyo ambayo ilinuia kugundua yanayoendelea nchini Mali, aligundua kuwa wapiganaji hao wanatumia sheria kali kwa wahalifu.

Hadi kufikia sasa, watu watatu wamenyongwa hadharani na wengine wanane kukatwa mikono huku wawili wakichapwa hadharani.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.