Miaka 10 baada ya mashambulio ya Bali

Imebadilishwa: 12 Oktoba, 2012 - Saa 12:08 GMT

Wengi wa wale waliouawa kwenye mashambulizi hayo walikuwa watalii kutoka Australia

Waziri mkuu wa Australia Julia Gillard, ameongoza kundi la wageni kutoka mataifa mbali mbali kuadhimisha miaka kumi ya mashambulizi ya kigaidi katika kisiwa cha Bali nchini Indonesia.

Miaka kumi iliyopita magaidi walishambulia maeneo mawili ya burudani kwa mabomu na kusababisha vifo vya raia 202 wakiwemo raia wa kigeni.

Nusu yao waliouwa watalii kutoka nchini Australian.

Waziri wa mambo ya nje wa Indonesia, Marty Natalegawa amesema kuwa shambulio hilo lilikuwa dhulma kubwa wa maisha ya binadamu

Bi Gillard alipongeza sana juhudi za uokozi zilizofanywa punde baada ya mashambulizi hayo pamoja na kuwakamata wale waliohusika.

Kwa sasa kisiwa cha bali kimerejelea katika hali yake ya kawaida huku taifa la Indonesia likijizatiti kukabiliana na athari za mashambulizi hayo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.