Mgomo wa wiki 3 wasitishwa Afrika Kusini

Imebadilishwa: 12 Oktoba, 2012 - Saa 11:25 GMT

Madereva waliokuwa wanagoma walifanya uharibifu mkubwa

Muungano wa vyama vya wafanyakazi nchini Afrika Kusini umeafikiana kusitisha mgomo wa madereva wa malori uliokuwa ukiendelea kwa muda wa wiki tatu.

Mgomo huo umechangia pakubwa uhaba wa bidhaa muhimu katika maduka ya jumla ikiwemo ukosefu wa mafuta ya petroli.

Mgomo wa madereva wa malori ulikuwa na athari kubwa kote nchini Afrika Kusini.

Licha ya kwamba vituo vya petroli vilikosa wanunuzi wa mafuta , pia usambazaji wa bidhaa katika maeneo mbali mbali ya nchi ulitatizika , ikiwa ni pamoja na vifaa vya hospitali.

Na pia kulikuwa na ghasia ambapo malori yalichomwa moto na dereva mmoja kuuawa kwa kutupiwa mawe na waandamanaji waliokuwa wanashiriki mgomo huo.

Kufikiwa kwa makubaliano hayo pia kutamaanisha kuwa mgomo uliotishiwa kufanywa na wahudumu wa bandari na reli umesitishwa

Lakini wimbi la migomo nchini Afrika Kusini bado halijaisha.

Bado kuna mzozo wa wafanyakazi kwenye migodi ya madini ambayo inatarajiwa kuanza labda wiki ijayo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.