Nchi zinazotumia Kifaransa zakutana

Imebadilishwa: 13 Oktoba, 2012 - Saa 14:48 GMT

Viongozi 20 wa mataifa yanayozungumza Kifaransa wanakutana katika Jamhuri ya Demokrasi ya Congo huku machafuko mashariki mwa nchi hiyo yanaendelea na kuna mzozo nchini Mali.

Rais Franois Hollande wa Ufaransa

Na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetaka nchi za Afrika Magharibi zipeleke maelezo kamili ya pendekezo lao la kuingia kijeshi nchini Mali, katika siku 45 zijazo, ili kuamua kama itatoa idhini au la.

Rais Francois Hollande wa Ufaransa aliuambia mkutano huo kwamba Ufaransa inaunga mkono pendekezo la kutuma jeshi la kimataifa Mali.

Piya alisema maswala muhimu kwa jumuia hiyo ni demokrasi na haki za kibinaadamu.

Hapo awali aliwakera wenyeji wake kwa kuwalaumu kwa rikodi yao katika maswala hayo.

Lakini alipigiwa makofi kwa kulaani mapigano ya mashariki mwa Congo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.