Cameroon yabanduliwa nje

Imebadilishwa: 14 Oktoba, 2012 - Saa 16:36 GMT
Wachezaji wa Cameroon

Wachezaji wa Cameroon

Cameroon leo imebadunduliwa nje ya fainali za kuwania kombe la mataifa bingwa barani Afrika zitakazo andaliwa nchini Afrika Kusini, licha ya kushinda mechi yao ya raundi ya pili kwa mabao mawili kwa moja dhidi ya Cape Verde hii leo mjini Yaunde.

Cape Verde iliilaza Cameroon kwa mabao mawili kwa bila katika mechi yao ya raundi ya kwanza.

Kabla ya mechi hiyo Cameroon ilihitaji kuishina Cape Verde kwa zaidi ya magoli mawili ili kujikatia tikiti ya kushiriki katika fainali hizo.

Cape Verde ambayo imeorodhesha nyuma ya Cameroon katika orodha ya timu bora ulimwenguni, imeandikisha historia kwa kufuzu kwa fainali hizo za kuwania kombe la mataifa bingwa barani Afrika kwa mara ya kwanza baada ya kuishinda Indomitable Lions kwa jumla la magoli matatu mwa mawili.

Katika mechi nyingine ya kufuzu, Ethiopia ilivaana na Sudan ambapo Ethiopia imeibuka na ushini wa mabao mawili kwa bila.

Katika mechi ya raundi ya kwanza Sudan ilishindakwa mabao matano kwa matatu.

Ethiopia sasa imufuzu kupitia sheria ya goli la ugenini baada ya timu hizo kufungana jumla ya magoli matano kwa matano.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.