Watu wauwawa Nigeria wakitoka msikitini

Imebadilishwa: 14 Oktoba, 2012 - Saa 16:19 GMT

Wakuu wa Nigeria wanasema kuwa watu waliokuwa na silaha wamewauwa watu kama 20 katika shambulio lilofanywa alfajiri kwenye kijiji cha Dogo Dawa katika jimbo la Kaduna kaskazini mwa nchi.

Kijiji cha Dogo Dawa kwenye ramani

Waliouwawa wengi walikuwa wakitoka msikitini.

Washambuliaji walifyatua risasi na kuwapiga visu waliokuwako na tena walimuuwa mzee wa jamii nyumbani kwake.

Afisa wa habari wa jimbo hilo, Saidu Adamu, aliiambia BBC kwamba gengi la majambazi wa jimbo hilo walifanya mauaji hayo.

Alisema shambulio hilo ni la kulipiza hatua iliyochukuliwa na wanakijiji cha Dogo Dawa ya kuunda kikosi cha wanamgambo wao wenyewe kuwatimua majambazi hao ambao wamekuwa tishio kijijini.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.