Syria yatumia mabomu ya cluster

Imebadilishwa: 14 Oktoba, 2012 - Saa 10:31 GMT

Shirika la kimataifa la kutetea haki za kibinaadamu, Human Rights Watch, limeishutumu Syria kuwa inazidi kutumia mabomu chane, yaani cluster bombs, dhidi ya raia.

Vita vya Syria

Shirika hilo linasema limeangalia video kwenye mtandao zinazodai kuonesha mabomu kama hayo 20 yakitumiwa sehemu mbali-mbali za Syria katika juma lilopita, ikilinganishwa na mwaka mmoja na nusu uliotangulia.

Akizungumza jana, mkurugenzi wa Umoja wa Mataifa wa Human Rights Watch, Philippe Bolopion, alisema inaonesha kuwa serikali haiwatii maanani kabisa wananchi wa Syria.

"Kwa muda tumekuwa tukishuku kuwa serikali ya Syria inatumia mabomu ya chane (yaani cluster bomb) lakini sasa tuna video na mashahidi kwamba serikali imetupa mabomu kama hayo kwenye maeneo ya makaazi kwa kutumia helikopta.

Kwa mfano imerusha mabomu hayo baina ya shule mbili.

Kwa hivo tunaamini kuwa serikali ya Syria inafaa kuacha haraka kutumia silaha za hatari zisokubalika kama hizi na isafishe maeneo yote ambako mabomu hayo yamemwagwa, na piya iwaarifu wakaazi wahusika juu ya hatari ya vibomu vidogo vilivotawanyika".

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.