Kiongozi wa 'MRC' akamatwa Kenya

Imebadilishwa: 15 Oktoba, 2012 - Saa 10:24 GMT

Wanachama wa vuguvugu la MRC

Polisi nchini Kenya wamewaua watu wawili wakati wa msako katika nyumba ya kiongozi wa kundi la MRC mjini Mombasa.

Kiongozi wa MRC au Mombasa Republican Council ambalo linataka kujitenga, Omar Mwamnuadzi, ikamatwa pamoja na wanachama wengine kumi na vuguvugu hilo.

Msako dhidi ya kundi hilo, unajiri huku kukiwa na wasiwasi kuwa huenda vurugu likatokea wakati wa uchaguzi mkuu utakaofanyika mapema mwaka ujao.

Mahakama kuu mjini Mombasa hivi maajuzi iliamua kuwa vuguvugu hilo ambalo linataka kujitengta kwa eneo la Pwani mwa Kenya sio haramu

Kundi hilo la MRC limekuwa likiilaumu serikali kwa madai ya kuwanyanyasa wakaazi wa pwani na kulitelekeza jimbo hilo zima.

Wakuu wa MRC pia wamekuwa wakisema hawaoni faida kutokana na rasilmali zilizoko pwani.

Kutokana na harakati zao wafuasi wengi wa MRC wamekuwa wakikawatwa na kushitakiwa kwa kuwa wanachama wa kundi haramu.

Baada ya mahakama kutoa uamuzi wa kulindolea kundi hilo marufuku iliyowekwa na serikali , serikali bado imekuwa ikiendelea kuwakamata vigogo wa vuguvugu hilo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.