Clinton ajilaumu kwa mashambulizi Libya

Imebadilishwa: 16 Oktoba, 2012 - Saa 08:44 GMT

Bi Hillary Clinton

Waziri wa nchi za kigeni wa Marekani Hillary Clinton amesema kuwa yeye ndiye aliyekuwa na jukumu la ulinzi katika ubalozi wa Marekani nchini Libya ambapo balozi wake aliuawa mwezi uliopita.

Mauaji ya balozi huyo Christopher Stevens pamoja na wamarekani wengine watatu limekuwa suala gumu sana katika siku hizi za mwisho za kampeini za uchaguzi wa urais.

Kamati maalum ya Congress imearifiwa kuwa ombi la kutaka kuongezewa uslama katika ubalozi huo lilikataliwa na idara ya serikali.

Bi Clinton aliambia vyombo vya habari nchini Marekani kuwa kuhakikisha usalama wa ubalozi wa Marekani kote duniani ni wajibu wake na wala sio wajibu wa Ikulu ya White house.

Tulichohitajika kufanya katika idara ya mambo ya ndani ilikuwa kuangazia kilichokuwa kinatokea wala sio kuhusu nini kitatokea, Bi Clinton aliambia waandishi wa habari.

''Na hilo ndilo nilikuwa naangazia usiku na mchana kujaribu kuhakikisha kuwa tunajaribu kudhibiti hali kwa ushirikiano na idara zengine za serikali.'' alisema Clinton

Serikali ya Rais Obama imekuwa ikikosolewa sana kuhusiana na shambulizi hilo dhidi ya ubalozi wa Benghazi hasa wakati huu ambapo kampeini za uchaguzi zinaposhika kasi.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.