Mbunge matatani kwa uchochezi Kenya

Imebadilishwa: 18 Oktoba, 2012 - Saa 10:39 GMT

Sheikh Mohammad Dor

Kiongozi moja mkuu wa kiisilamu nchini Kenya, ambaye pia ni mbunge mteule ameshtakiwa kwa kuchochea ghasia.

Mbunge Sheikh Mohammad Dor alisema kuwa anajitolea kufadhili vuguvugu la MRC linalotaka kujitenga kwa eneo la Pwani.

Hatua ya kushtakiwa kwa Sheikh Mohammed Dor inakuja siku tatu baada ya kukamatwa kwa kiongozi wa kundi hilo Omar Mwamnuadzi.

Sheikh Dor alikamatwa jana jioni baada ya kutangaza hadharani kuwa anaweza kufadhili vuguvugu hilo, ingawa aliachiliwa asubuhi ya leo kwa dhamana ya dola 23,000 baada ya kukana mashtaka ya uchochezi.

Wanachama wa MRC wanaotaka kujitenga na Kenya

Kesi yake itaanza kusikilizwa tarehe kumi na tatu mwezi Novemba.

Sheikh Dor ambaye amelaani msako unaoendelea wa polisi dhidi ya kundi hilo mjini Mombasa, alisema kuwa kundi hilo ambalo mahakama ilisema kuwa sio haramu, kwa mtu kuamua kulifadhili sio kosa.

Dor ni mmoja wa wabunge kumi na wawili wa Kenya ambao hawakuchaguliwa ingawa waliteuliwa kuwakilisha maswala kadhaa bungeni.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.