Berlusconi mahakamani kwa kesi ya kimapenzi

Imebadilishwa: 19 Oktoba, 2012 - Saa 15:53 GMT

Aliyekuwa waziri mkuu wa Italia Silvio Berluscon akitoka mahakamani kuhusiana na kesi ya dhulma ya kimapenzi

Aliyekuwa waziri mkuu wa Italia Silvio Berlusconi amejitokeza kwa nadra katika mahakama ya Milan aliposhtakiwa kwa makosa ya kumlipa msichana aliye na umri mdogo fedha ili afanye naye mapenzi.

Bwana Berlusconi ameiambia mahakama kuwa hajawahi kuwa na uhusiano wowote wa kimapenzi na msichana huyo Karima El-Mahroug, mcheza dansi aliye mzaliwa wa Morocco.

Alikuwa na umri wa miaka kumi na saba alipohudhuria sherehe binafsi ya Bwana Berlusconi lakini Berlusconi anasema aliamini kuwa alikuwa na umri wa miaka 24 kama alivyomwambia.

Upande wa mashitaka unadai kuwa mikusanyiko hiyo ilikuwa ni ya kukutanika kufanya ngono madai amabayo Bwana Berlusconi anakanusha.

Berlusconi pia anashutumiwa kutumia madaraka yake vibaya kwa kuwaamuru polisi kumtoa kizuizini msichana huyo alipokamatwa kwa makosa mengine.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.