Wameuawa wakienda harusini Afghanistan

Imebadilishwa: 19 Oktoba, 2012 - Saa 10:06 GMT

Shambulizi la bomu nchini Afganistan

Shambulizi kubwa la bomu limewaua watu 18 wakielekea harusini nchini Afghanistan.

Takriban watu wengine 15 wamejeruhiwa katika kile kinachosemekana kuwa mojawapo ya mashambulizi mabaya kutokea nchini humo kwa muda mrefu.

Basi ndogo lililokuwa limewabeba wanaume, wanawake na watoto kuelekea harusini wilayani Balkh, lilishambuliwa likiwa safarini.

Haijulikani ikiwa gari hilo lililengwa kwa mashambulizi au ilikuwa bahati mbaya tu wakati bomu liliokuwa limetegwa kando ya barabara lilipuka.

Hadi sasa hakuna yeyoye amewajibikia shambulizi hilo.

Maafisa wanasema kuwa wanatarajia idadi ya waliofariki kuongezeka.

Eneo la Kaskazini mwa Afghanistan limekuwa mojawapo ya maeneo salama nchini humo kwa miaka kumi iliyopita tangu Marekani kuvamia nchi hiyo.

Lakini wapiganaji wa Taleban wamekuwa wakiongeza kasi harakati zao katika eneo hilo. Wanajeshi wa NATO licha ya idadi yao kubwa wameshindwa kuangamiza wapiganaji hao.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.