Mlipuko wa Virusi vya Marburg Uganda

Imebadilishwa: 19 Oktoba, 2012 - Saa 17:22 GMT

Virusi vya Marburg vinafanana na vile vinavyosababisha Ebola

Wizara ya afya nchini Uganda imeonya dhidi ya mlipuko wa virusi vikali vinavyosababisha ugonjwa wa Marburg katika eneo la Kusini Magharibi mwa nchi.

Katika taarifa ya wizara hiyo, maafisa wamesema kuwa uchunguzi wa maabara ulithibitisha kuwa watu wawili wa familia moja walifariki kutokana na virusi hivyo wilayani Kabale.

Jamaa wengine wa familia hiyo, wanaaminika kufariki kutokana na ugonjwa huo mapema mwezi huu.

Virusi vya Marburg, ambavyo vinaaminika kuwa na dalili sawa na homa ya Ebola na huambukizwa katika njia moja, kupitia majimaji ya mwilini mfano jasho, mate na hata damu pamoja na kuwashika wanyama waliombukizwa na homa hiyo.

Hata hivyo ugonjwa huo hauna tiba.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.