Mapigano yarudi Darfur

Imebadilishwa: 20 Oktoba, 2012 - Saa 15:10 GMT

Wakuu wa Sudan wanasema watu kadha wamekufa kwenye shambulio lilofanywa na wapiganaji dhidi ya wanajeshi wa serikali katika eneo la Darfur, magharibi mwa nchi.

Kikosi cha usalama cha UMoja wa Mataifa na Afrika huko Darfur

Afisa mmoja wa serikali alisema wanamgambo wanaounga mkono serikali wameuliwa katika shambulio hilo la ghafla, karibu na al-Fasher, mji mkuu wa jimbo la North Darfur.

Umoja wa wapiganaji - Sudanese Revolutionary Front - ulisema ulifanya shambulio hilo na kuuwa wanajeshi wa serikali na kuteka magari ya jeshi na silaha.

Baadhi ya makundi ya wapiganaji ya Darfur mwaka jana yalitia saini mkataba wa amani na serikali ya Sudan, lakini makundi mengine yanaendelea kupigana.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.