Vikwazo vya UN dhidi ya M23 vyakaribia

Imebadilishwa: 20 Oktoba, 2012 - Saa 13:42 GMT

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linakusudia kuliwekea vikwazo kundi la M23 linalopigana mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo.

Rais Joseph Kabila wa DRC akihutubia Baraza kUu la UMoja wa Mataifa mwezi Septemba

Taarifa iliyotolewa na baraza hilo inasema nchi zinazovunja vikwazo dhidi ya kupeleka silaha eneo hilo, nazo piya zitawekewa vikwazo.

Hakuna nchi iliyotajwa jina, lakini lakini ripoti ya jopo la watalamu wa Umoja wa Mataifa imesema kuwa Rwanda na Uganda zinapeleka silaha kwa wapiganaji na msaada mwengine wa kijeshi.

Taarifa hiyo bado haikuwa azimio la Umoja wa Mataifa, lakini inalaani kundi la M23 kwa kushambulia raia na kujaribu kuanzisha utawala wake mashariki mwa Congo.

Taarifa inasema Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linakusudia kuweka vikwazo maalumu kulenga viongozi wa M23 na wengine wanaokwepa vikwazo vinavyokataza silaha kuingizwa Congo.

Taarifa hiyo haikuitaja Rwanda kwa jina, ambayo imeshutumiwa na wataalamu wa Umoja wa Mataifa kuwa inaongoza mapigano ya mashariki mwa Congo, pamoja na Uganda inayoshutumiwa kuwapatia wapiganaji silaha.

Lakini inalaani vikali msaada wowote ambao M23 inapata, na inaeleza wasiwasi mkubwa kwamba kuna ripoti kuwa zinatoa msaada huo.

Taarifa hiyo imetolewa siku moja baada ya Rwanda kuchaguliwa na nchi nyingi kushika kiti kwa muda katika Baraza hilo la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.