Njama ya mapinduzi yapikwa Guinea Bissau

Imebadilishwa: 21 Oktoba, 2012 - Saa 17:24 GMT

Duru za jeshi la Guinea Bissau, Afrika Magharibi, zinaeleza kuwa watu waliokuwa na silaha wameuwawa kwenye shambulio dhidi ya kambi ya jeshi nje ya mji mkuu, Bissau.

Guinea Bissau

Inaarifiwa mapambano yaliendelea kwa saa nzima.

Waandishi wa habari wanasema shambulio hilo lilofanywa usiku wa manane, litazidisha wasiwasi Guinea Bissau, ambako jeshi lilipindua serikali mwezi wa Aprili.

Fujo za mara-kwa-mara nchini Guinea Bissau zimeifanya nchi hiyo kuwa pahala pa kupitisha magendo ya mihadarati, baina ya Amerika Kusini na Ulaya.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.