AMISOM itauhama uwanja wa Mogadishu

Imebadilishwa: 21 Oktoba, 2012 - Saa 09:27 GMT

Kikosi cha amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia, AMISOM, kimekubali ombi la Shirika la Kandanda la Somalia kuhama kutoka uwanja wa mpira wa Mogadishu, ili uwanja huo upate kufanyiwa ukarabati kuweza kutumiwa tena kama pahala pa michezo.

Mogadishu stadium

Msemaji wa AMISOM, Kanali Ali Adan Hamud, alisema AMISOM imekaribisha ombi hilo na kwamba AMISOM imeamua kuondoka kwenye uwanja huo ufikapo mwezi wa Disemba mwaka huu.

Uwanja huo umekuwa kambi ya askari wa AMISOM tangu Agosti mwaka jana.

Kabla ya hapo ukitumiwa na wapiganaji wa Al-Shabab na mapambano makali yamewahi kutokea kwenye eneo la uwanja huo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.