Njama ya al-Qaeda yatibuliwa Jordan

Imebadilishwa: 22 Oktoba, 2012 - Saa 07:25 GMT

Mmoja wa washukiwa wa ugaidi waliokamatwa na maafisa wa Jordan

Maafisa nchini Jordan, wamethibitisha kuwakamata wapiganaji 11 wanaodaiwa kupanga njama ya mashambulizi dhidi ya wanadiplomasia wa nchi za Magharibi pamoja na maduka katikakati mwa mji mkuu Amman.

Msemaji wa serikali, Samih Maayta alisema kuwa washukiwa hao walikamatwa siku chache zilizopita na kwamba wangali wanazuiliwa.

Aidha bwana Maayta alisema kuwa washukiwa hao waliingiza silaha katika nchi jirani ya Syria na kwamba wapiganaji wengine wa al-Qaeda nchini Iraq, waliwasaidia kutengeza mabomu nyumbani.

Njama yao ilianza kupangwa tangu mwezi Juni

Maafisa wa ujasusi waliwapiga darubini siku nyingi kuchungza mienendo ya washukiwa hao waliokuwa wanapanga njama hiyo ikiwemo utafiti wao wa mabomu.

Afisaa huyo aliambia BBC kuwa hiyo ilikuwa njama ya al-Qaeda, ya shambulizi waliokuwa wanapanga kufanya tarehe tisa Novemba kuadhimisha shambulizi walilolifanya mjini Amman mwaka 2005.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.