Mkuu wa mashtaka ICC Fatou Bensouda awasili Kenya

Imebadilishwa: 22 Oktoba, 2012 - Saa 12:21 GMT

Mwendesha mkuu wa mashtaka ICC Fatou Bensouda

Mwendesha mkuu wa Mashtaka katika mahakama ya kimataifa ya ICC Fatou Bensouda, yuko nchini Kenya, kufanya mazungumzo kuhusu ghasia za baada ya uchaguzi zilizokumba nchi hiyo mwaka 2008.

Zaidi ya watu elfu moja waliuawa kwenye ghasia hizo.

Akiongea akiwa mjini Nairobi, Bi Bensouda alisema kuwa atakutana na viongozi wa kisiasa pamoja na wananchi wa kawaida wakati wa ziara yake ya siku tano.

Ziara hii inakuja kabla ya kuanza kwa kesi za washukiwa wakuu wa ghasia hizo walioshtakiwa kwa uhalifu dhidi ya bindamu mwaka ujao.

Bensouda amesema kuwa washukiwa wa ghasia za baada ya uchaguzi lazima wakabiliwe na sheria.

Wawili miongoni mwa watu walioshtakiwa , Naibu waziri mkuu Uhuru Kenyatta na mbunge William Ruto wametangaza azma yao ya kugombea urais katika uchaguzi ujao mwaka ujao.

Alisema kuwa kesi za washukiwa hao mjini Hague, zitaendelea licha ya matokeo ya uchaguzi mkuu akisema kuwa majaji wana ushahidi wa kutosha kuendesha kesi za washukiwa hao.

Alisisitiza kuwa sio watu wa Kenya wala serikali au kabila lolote wako kizimbani lakini ICC itaendesha kesi yake kwa haki na usawa dhidi ya washukiwa wakuu.

Akiwa Kenya, atazuru vitovu vya ghasia za baada ya uchaguzi na hata kukutana na watu waliopoteza makao yao wakati wa ghasia hizo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.