BBC imekana kuingilia ripoti ya dhulma

Imebadilishwa: 23 Oktoba, 2012 - Saa 13:17 GMT

Jimmy Saville

Mkurugenzi wa shirika la BBC, George Entwistle,amekanusha madai kuwa wahariri wakuu walishinikizwa kutopeperusha ripoti ya dhulma za kimapenzi dhidi ya watoto inayomkabili mtangazaji wa usiku, hayati Jimmy Savile.

Aidha Entwistle amewaambia wabunge kuwa kauli ya kutoipeperusha ripoti hiyo ilitokana na mawasiliano tata baina ya vitengo ndani ya BBC wala haikuwa sera ya shirika.

Uchunguzi huu umezua utata kuhusu taaluma ya uanahabari katika BBC.

Maafisa wa polisi wanaendelea kuchunguza kashfa ya mtangazaji huyo aliyehudumu kwa siku nyingi.

George Entwistle aliambia Wabunge kuwa aliamini kwamba uchunguzi wa mienendo ya Jimmy Saville haukupaswa kusitishwa. Lakini alikanusha kuwa kulikuwa na njama ya kuficha ukweli.

Alisema anaamini kuwa kipindi cha Newsnight hakikushinikizwa na wakuu wa BBC kubana uchunguzi wake juu ya nyota huyo wa zamani.

Lakini alilaumu alichoita kukatika kwa mawasiliano miongoni mwa waandishi wa habari wa kipindi hicho.

Juu ya madai juu ya uwezekano wa Jimmy Seville kuendelea kuwanyanyasa kimapenzi watoto wadogo kwa miongo kadhaa, Mkuu wa BBC alikiri kuwa hali hiyo imeharibia BBC sifa. Alisema kuwa kulikuwa na utamaduni mbaya katika BBC miaka ya 60 na 70.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.