Njama ya kumuua Rais wa Benin yatibuka

Imebadilishwa: 23 Oktoba, 2012 - Saa 10:25 GMT

Rais Boni Yayi

Watu watatu wamekamatwa kufuatia njama ya kumuua Rais wa Benin Thomas Boni Yayi kwa kumpa sumu. Taarifa hii ni kwa mujibu wa maafisa wa serikali ya Benin.

Kiongozi wa mashtaka, Justin Gbename alisema kuwa washukiwa ni pamoja na mpwa wa rais Yayi , daktari wake na waziri wa zamani.

Aliongeza kuwa wale waliozuiliwa wanakabiliwa na makosa ya jinai na jaribio la kumuua Rais Boni.

Bwana Yayi, aliyekuwa mfanyakazi wa zamani wa benki, alichukua mamlaka mwaka 2006 na ni mwenyekiti wa Muungano wa Afrika

Viongozi wa mashtaka wamewataja washukiwa hao ambao ni waziri wa zamani wa biashara Moudjaidou Soumanou, Daktari Ibrahim Mama Cisse na Zouberath Kora-Seke,mpwa wa rais huyo ambaye alifanya kazi katika makao yake.

Maafisa wanasema kuwa pia watajitayarisha kutoa vibali vya kukamatwa kwa mfanya biashara Patrice Talon, mshirika wa zamani wa Rais huyo ambaye walitofautiana naye.

Dalili zilijitokeza baada ya rais kuanza kutapika na kuwa mlegevu kulingana na mwandishi wa BBC mjini Cotonou.

"tunashakuru njama hiyo haikufanikiwa'' alisema kiongozi wa mashtaka bwana Gbenameto.

"Zouberath alizungumzia jaribio la kumuua rais kwa jamaa zake na hao ndio waliomdokezea rais kuhusu njama hiyo."

Aliongeza kuwa viongozi wa mashtaka wametaka washukiwa kufunguliwa mashtaka ya jinai na jaribio la mauaji.

Bwana Yayi alishinda uchaguzi mkuu mwezi Machi mwaka 2006 na kushinda muhula mwingine mwaka jana.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.