Bomu lawaua wafungwa A. Kusini

Imebadilishwa: 23 Oktoba, 2012 - Saa 10:41 GMT

Bendera ya Afrika Kusini

Polisi nchini Afrika Kusini wanasema kuwa watu wawili wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa vibaya baada ya bomu kulipuka karibu na gari lililokuwa likiwasafirisha wafungwa mjini Johannesburg.

Msemaji wa Polisi amethibitisha vifo hivyo na kuongeza kuwa mlipuko ulitokea kwenye gari moja lililokuwa likiwasafirisha mahabusu kutoka mahakama ya Randburg kwenda gerezani pembeni mwa mji wa Johannersburg.

Ilikua majira ya jioni pale gari la polisi lilipokua linawarejesha kwenye jela kuu ya Joburg wafungwa 36 kutoka Mahakama ya Randburg bada ya kusikiliza kesi zao kwa makosa mbali mbali, ndipo mlipuko ulipotokea ndani ya gari hilo lilipo karibia lango la jela kuu na kuwauwa wafungwa 3 .

Mwandishi wa BBC mjini Johannesburg Omar Mutasa anasema kuwa wafungwa 15 walijeruhiwa kutokana na mlipuko huo na wamelazwa katika hospitali mbali mbali mjini Johannesburg wakiwa chini ya ulinzi mkali wa Polisi na maafisa wa magereza.

Msemaji wa Polisi ya Afrika Kusini Neville Malila, hakuwa na maelezo zaidi ila Kusema wanakwenda kuchunguza tukio hilo la aina yake kutokea kwa mara ya kwanza wafungwa kujaribu kutoroka wakitumia vifa vinavyo lipuka .

Jela ya Johannesburg (SunCity) ipo karibu na migodi ya madini panapotumiwa vilipuzi vya Dynamite na kwa upande mwengine kuna kambi ya kijeshi karibu na jela hio

Bado haijajulikana mlipuko huo ikiwa ulitokana na bomu la kurushwa kwa mkono mabomu yanayotumiwa kwenye migodi

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.