Barua pepe yenye utata kuhusu Benghazi

Imebadilishwa: 24 Oktoba, 2012 - Saa 08:55 GMT

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton aliwajibika na kusema kuwa wizara yake ndiyo inahusika na usalama wa balozi za Marekani kote duniani

Shirika la bahari la Reuters limesema, limepata barua pepe ambayo inaonyesha kuwa maafisa katika Ikulu ya White House waliambiwa punde baada ya shambulizi dhidi ya ubalozi wa Marekani nchini Libya kuwa kundi la wapaiganaji wa kiisilamu walikiri kufanya shambulizi hilo.

Kulingana na barua pepe hiyo,maafisa wa idara ya mambo ya ndani ya serikali ya Marekani walishauri kuwa kundi la wapiganaji wa Libya, Ansar al-Sharia lilikiri kufanya mashambulizi hayo.

Balozi wa Marekani mjini Benghazi na wamarekani wengine watatu waliuawa kwenye mashambulizi hayo.

Kwa wiki kadhaa, Ikulu ya Marekani ilidaiwa kutoa habari za kupotosha kuhusiana na shambulizi hilo, wakisema kuwa ghasia zilitokana na vurugu za ghafla dhidi ya filamu ya Marekani iliyokejeli dini ya kiisilamu.

Maafisa nchini Libya waliwakamata washukiwa kadhaa wa machafuko hayo yaliyosababisha kifo cha balozi wa Marekani nchini humo pamoja maafisa wengine wa ubalozi huo mjini Benghazi.

Waziri mkuu mpya wa Libya Mustafa Abu Shaqur aliambia BBC kuwa uchunguzi unaoendelea kuhusiana na kisa hicho kutafuta wahusika zaidi.

Shambulizi lilifanyika wakati wa maandamano yaliyopinga filamu iliyotengezwa nchini Marekani kumkejeli Mtume Mohammed.

Maandamano sawa na hayo yalisambaa katika nchi za kiarabu na mataifa ya Kaskazini mwa Afrika.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.