Sudan yalaumu Israel kwa mashambulizi

Imebadilishwa: 25 Oktoba, 2012 - Saa 11:57 GMT

Kiwanda cha silaha kilicholipuka Sudan

Serikali ya Sudan inasema inaamini kuwa Israel ndiyo iliyoshambulia kiwanda chake cha silaha na kusababisha milipuko mikubwa iliyotokea hapo jana.

Kiwanda hicho ni cha kutengeza silaha za jeshi la Sudan Kaskazini.

Serikali ya Sudan imesema kuwa inaamini Israel ilihusika na milipuko iliyotokea katika kiwanda hicho mjini Khartoum siku ya Jumanne.

Waziri wa utamaduni na mawasiliano Ahmed Bilal Osman, alisema kuwa waisraeli wanne walishambulia kiwanda cha silaha na kuwaua watu wawili. Bado Israel haijatoa tamko lolote kuhusu madai dhidi yake.

Sudan imewahi kulaumu Israel kwa mashambulizi kama hayo katika siku za nyuma.

Duru zinasema kuwa Israel inaamini silaha zinapitishwa katika eneo hilo zikiingizwa Gaza.

Nyaraka za siri za Marekani zilizofichuliwa miaka mitatu iliyopita , ilionyesha kuwa Sudan ilikuwa iningiza kisiri silaha za Iran katika ukanda wa Gaza.

Mwezi Aprili mwaka jana, Khartoum pia ilidai kuwa Israel ndiyo ilifanya shambulizi la angani ambalo liliwa watu waili karibu na mji wa Port Sudan. Israel, kwa mara nyingine haikutoa tamko lolote kuhusu madai hayo.

Mlipuko huo ulisababisha moto mkubwa na milipuko zaidi ilifuatia wakati wazima moto walifika kujaribu kuudhibiti moto huo, uliozuka kutoka kampuni hiyo ya Yarmouk .

Gavana wa eneo hilo (Abdul Rahman Al-Khider Rahman) amesema watu kadha walijeruhiwa na kupelekwa hospitalini baada ya kuvuta moshi.

Mlipuko wa kwanza ulitokea katika hifadhi ya silaha na bado chanzo chake kinachunguzwa. Vifaa vingi vya kijeshi viko karibu na kampuni hiyo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.