Mwandishi mwengine auawa Somalia

Imebadilishwa: 24 Oktoba, 2012 - Saa 14:08 GMT

Hali ya Somaliland imekuwa tulivu ikilinganishwa na Somalia

Mwandishi wa habari katika jimbo lililojitenga na Somalia, Somaliland, ameuawa na watu waliokuwa wamejihami alipokuwa anarejea nyumbani kutoka kazini.

Ahmed Farah Ilyas alikuwa mwandishi katika eneo Las Anod, mji ambao umekumbwa na msukosuko akifanyia kazi kampuni ya Somalia ya Universal TV.

Kabla ya kuuwawa kwake, Farah alikuwa anafuatilia taarifa ya mlipuko wa mabomu ya ardhini ambayo serikali imelaumu Al Shabaab kulifanya.

Ilyas ni mwandishi habari wa kumi na sita kuuawa nchini Somalia mwaka huu.

Tangu kuong'olewa mamlakani kwa Rais Siad Barre mwaka 1991, Somalia daima imeshuhudia wanamgambo wa Somalia wakipigania udhibiti wa Somalia.

Somaliland ilijitangazia uhuru wake baada ya kung'olewa kwa Barre na imekuwa salama ikilinganishwa na Somalia.

Eneo la Sool liko katika sehemu ambayo inadaiwa na jimbo la Puntland na imeshuhudia msukosuko siku za hivi karibuni.

Mwandishi wa BBC Hagar Jibril ambaye yuko katika eneo jirani la Burao, anasema kuwa watu walishuhudia tukio hilo wanasema Ilyas alipigwa risasi na watu wawili waliokuwa wamejihami nyakati za jioni.

Mapema siku ya Jumanne, watu wanne walijeruhiwa baada ya kulipukiwa na mabomu ya kutega ardhini ambayo gavana wa eneo la Sool Mahamed Mahamud Ali alisema yalitegwa na Al Shabaab.

Duru zinaarifu kuwa kesi dhidi ya wanamgambo hao ilianza kusikilizwa mjini Las Anod siku ya Jumanne.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.