Fatou Bensouda akutana na wakimbizi Kenya

Imebadilishwa: 25 Oktoba, 2012 - Saa 09:10 GMT

Wakati wa ziara yake nchini Kenya Bensouda pia alikutana na Rais Mwai Kibaki na Waziri Mkuu Raila Odinga

Nchini Kenya. mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya jinai- ICC, Fatou Bensouda leo atatembelea kambi za wakimbizi wa ndani walioathirika na mapigano baada ya uchaguzi wa 2007.

Wakenya wanne wameshtakiwa katika mahakama ya ICC kwa madai ya kuhusika katika mapigano hayo yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu alfu moja, na wengine laki sita kuachwa bila makao.

Bi Bensouda, ambaye yuko Kenya kwa siku tano, anaanzia ziara yake katika kambi ya Naivasha kabla ya kuelekea mjini Eldoret, mojawapo ya maeneo yaliyoshuhudia vurugu kubwa wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi nchini Kenya.

Bensouda yuko nchini Kenya kukutana na wakimbizi wa ghasia hizo ambao baadhi bado wako katika kambi za muda miaka minne baada ya ghasia hizo.

Atasikiliza masaibu yao na tayari amesema kuwa nia yake ni kuwatendea haki wakimbizi hao katika kesi zitakazofanyika huko Hague.

Bensouda alikutana na viongozi wengine akiwemo Rais Mwai Kibaki na waziri mkuu Raila Odinga.

Tayari amesisitiza kuwa kesi za washukiwa wa ghasia hizo sio hukumu yoyote dhidi ya umma wa Kenya bali ni dhidi ya washukiwa pekee yao.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.