Mkuu wa kampuni ya Anglo American kujiuzulu

Imebadilishwa: 26 Oktoba, 2012 - Saa 10:38 GMT

Cynthia Carroll

Cynthia Carroll anatarajiwa kujiuzulu kama afisaa mkuu mtendaji wa kampuni ya madini ya Anglo American baada ya kuhudumu kwa miaka sita.

Mapema mwaka huu wamiliki wa kampuni hiyo walielezea kutofurahishwa na kudorora kwa faida za kampuni na kumtaka mwenyekiti kumwajiri afisaa mkuu mtendaji mpya.

Kampuni hiyo hata hivyo imesema ulikuwa uamuzi wa Cythia kuacha kazi huku mwenyekiti Sir John Parker akimsifu kwa kazi yake.

Lakini kampuni haijatangaza tarehe rasmi ya kuacha kazi kwa Cynthia. Hatua hii itawaacha tu wanawake wawili wakiwa wakuu wa makampuni mawili makubwa nchini Uingereza.

Wanawake hao ni pamoja na Angela Ahrendts katika kampuni ya Burberry na Alison Cooper wa Imperial Tobacco.

Hisa za kampuni hiyo zilipanda juu kwa asilimia mbili katika soko la hisa la London, lakini baadaye thamani ya hisa zake ilishuka kwa miezi minane iliyopita.

Cynthia alisema kuwa ulikuwa uamuzi mgumu kuacha kazi.

Cynthia alikabiliwa na shinikizo kutoka kwa wamiliki wa kampuni hiyo baada ya kampuni yake nchini Afrika Kusini kukumbwa na migomo katika mgodi wake wa Platinum wafanyakazi wakitaka kulipwa mishahara mizuri na kuwepo mazingira bora ya kazi

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.