Wanyama kuihama Celtic

Imebadilishwa: 26 Oktoba, 2012 - Saa 16:31 GMT
Victor Wanyama

Victor Wanyama

Mcheza kiungo wa timu ya taifa ya Kenya, Harambee stars, anayeichezea klabu ya Celtic ya Scotland Victor Wanyama, anaripotiwa kudinda kusaini kandarasi mpya na klabu hiyo ya Celtic.

Kandarasi ya wanyama na klabu hiyo ya Celtic inatarajiwa kukamilika mwaka wa 2015, na klabu hiyo ilikuwa na matarajio ya kuumpa mchezaji huyo kandarasi mpya, ili kuzuia uwezekano wa mchezaji huyo kuhamia vilabu vingine, vinavyoshiriki kwenye ligi kuu ya Premier ya England ambavyo vimeonyesha nia ya kumsajili kama vile Manchester United.

Lakini Wanyama mwenye umri wa miaka 21 na ambaye alijiunga na Celtic kutoka kwa klabu ya Beerschot ya Ubelgiji mwaka wa 2011, haamini kuwa kandarasi hiyo mpya inawiana na dhamani yake kwa sasa na hivyo amekataa kuisaini.

Kwa mujibu wa agenti wa Wanyama, Rob Moore, tayari Celtic imefahamishwa kuwa kandarasi hiyo haikithi matarajio ya mchezaji huyo.

Ripoti zinasema klabu hiyo ya celtic ilikataa ombi kutoka kwa vilabu kadha ambavyo vilikuwa vikitaka kumsajili mchezaji huyo mapema mwaka huu.Kuna fununu kuwa huenda mchezaji huyo akahamia England msimu ujao wa usajili na miongoni mwa vilabu ambavyo vimeonyesha nia ya kumsajili ni pamoja na Manchester United,Manchester City na Tottenham.vic

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.