Arsenal yaandikisha ushindi

Imebadilishwa: 27 Oktoba, 2012 - Saa 17:57 GMT
Kipa wa Arsenal

Kipa wa Arsenal

Mikel Arteta ameinusuru timu yake ya Arsenal kwa kufunga bao moja kunako dakika za mwisho za mechi yao na Queens Park Rangers.

Ushindi huo pia ulikuwa mwanzo mpya kwa Jack Wilshere ambaye alikuwa anarejea uwanjani baada ya kuwa nje kwa zaidi ya mwaka mmoja kutoka na jeraha.

Kufuatia ushindi huo Arsenal sasa imepanda hadi nafasi ya nne, katika msururu wa ligi kuu premier na alama 15 alama 7 nyuma ya vinara Chelsea, ambao wanacheza dhidi ya Manchester United hapo kesho.

Katika mechi nyingine Wigan iliandishia ushindi wake wa kwanza katika nyumbani msimu huu baada ya kuilaza West Ham kwa mabao mawili kwa moja.

Ivan Ramis aliifungia West Ham bao lake la kwanza naye James McAthur akifunga bao la ushindi.zaidi ya vipande kuweka.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.