Berlusconi asema atabaki kwenye siasa

Imebadilishwa: 27 Oktoba, 2012 - Saa 15:20 GMT
Silvio Berlusconi

Waziri Mkuu wa zamani wa Utaliana, Silvio Berlusconi, anasema anaona anawajibika kubaki kwenye siasa ingawa amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja kwa kuhepa kodi ya mapato.

Bwana Berlusconi alisema amekutikana na makosa kwa misingi ya kile alichosema ni ndoto; na kwamba inambidi aendelee na siasa apate kubadilisha mfumo wa mahakama ili kuhakikisha kuwa yaliyomkuta yeye, hayatatokea kwa wengine.

Waandishi wa habari wanasema tangazo hilo limeshangaza kwa sababu mapema juma hili Bwana Berlesconi alisema hataongoza chama chake kwenye uchaguzi wa mwakani.

Wakili wa Bwana Berlusoni anasema atakata rufaa.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.