Kamanda "Gordon" auwawa Somalia

Imebadilishwa: 28 Oktoba, 2012 - Saa 18:41 GMT
Jeshi la Somalia na AMISOM waonyesha silaha walizopata kutoka al-Shabaa, Mogadishu

Kamanda mwanadamizi wa Somalia ameuwawa alipoviziwa na kushambuliwa na kundi la wapiganaji wa Kiislamu, Al Shabaab.

Gavana wa jimbo la Shabelle Kusini, kusini mwa Somalia, alisema Jenerali Ibrahim Mohamed Farah Gordon na wanajeshi wengine watatu waliuwawa karibu na mji wenye bandari, mji wa Merca.

Al Shabaab - ambao wanadhibiti eneo karibu lote la kusini na kati mwa Somalia - hivi karibuni waliondoka katika miji yote mikubwa, pamoja na Merca.

Kundi hilo bado linafanya mashambulio ya kuvizia na mengineyo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.