Viongozi wa Kopti wamchagua Papa mpya

Imebadilishwa: 29 Oktoba, 2012 - Saa 11:02 GMT

Mazishi ya Papa Shenouda yalifanyika mapema mwaka huu

Baraza la maaskofu wa Kikopti nchini Misri, linatarajiwa kumpigia kura mrithi wa papa Shenouda wa tatu aliyefariki mwezi Machi.

Maaskofu wawili na watawa watatu wako kwenye orodha ya wale wanaogombea wadhifa huo ambapo yeyote atakayeshinda atakuwa kiongozi wa miamoja na kumi na nane kuongoza madheheyo hayo ambayo ndio kundi ndogo sana la wakristo duniani.

Baraza hilo litachagua wagombea watatu na kuandika majina yao kwenye vijikaratasi ambavyo vitawekwa kwenye boxi katika mimbar ya kanisa la mtakakatifu Mark, mjini Cairo.

Kisha mtoto atakayekuwa amefumbwa macho, atachukua kijikaratasi kimoja kutoka kwenye boxi hilo, jina la atakekuwa amechukua ndiye atakuwa Papa mpya.

Atayakuchaguliwa ataapishwa katika sherehe itakayofanyika tarehe 19 mwezi Novemba.

Papa Shenouda wa tatu aliongoza waumini wa kanisa hilo nchini Misri kwa miongo minne na alifariki akiwa na umri wa miaka 88 mwezi Machi, baada ya kuugua saratani.

Aliwataka maafisa wa kanisa hilo kufanya kila wawezalo kushughulikia maswala muhimu ya waumini wa kanisa hilo baada ya mashambulizi kadhaa dhidi ya makanisa katika miaka ya hivi karibuni.

Mrithi wake anakabiliwa na kibarua cha kuwahakikishia kuimarika kwa imani jamii ya waumini wa kanisa hilo hasa wakati huu ambapo harakati za makundi ya kiisilamu zimeshika kasi nchini Misri.

Vijana wengi wa kikopti watakuwa wanatazamia kupata kiongozi atakayewasaidia kuweka bayana majukumu yao chini ya utawala usio kuwa wa Mubarak.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.