Arsenal yanusurika

Imebadilishwa: 1 Novemba, 2012 - Saa 14:49 GMT
Theo Walcott Akisherehekea bao lake

Theo Walcott Akisherehekea bao lake

Kocha wa Arsene Wenger, amekiri kuwa ushindi wao wa mabao 7-5 dhidi ya Reading siku ya Jumanne usiku, wakati wa mchuano wa kombe la Ligi uliwanusuru kutoka kwa maangazi makubwa.

Amesema amefurahishwa sana na jinsi wachezaji wake walivyojitahidi wakati wa mechi hiyo kwa kutoka nyuma ya kufungwa mabao 4-0 kufikia wakati wa mapunziko.

Katika kipindi cha pili Arsenal, ilifunga mabao manne hatua iliyopelekea mechi hiyo kuongezwa muda wa ziada.

Theo Walcott alifunga mabao matatu naye Marouane Chamakh alifunga mawili na kusaidia Arsenal kufuzu kwa raundi ya tatu.

"Tulitoka kwenye wimbi la aibu na kuibuka na ushindi ambao haukutarajiwa na zaidi ya yote heshima na hadhi miongoni mwa mashabiki wetu ambao walikuwa wamekata tamaa" alisema Wenger.

Kocha wa Reading Brian McDermott, amesema matokeo hayo ndio mabaya zaidi tangu alipoanza kazi ukufunzi.

Baada ya dakika 35, Arsenal tayari ilikuwa imelazwa mabao manne lakini Walcott aliifunguia Arsenal bao lake la kwanza muda mfupi kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika.

Lakini baada ya dakika Tisini za mechi kumazika, timu hizo mbili zilikuwa zikitoshana nguvu ya mabao 4-4.

Dakika chache baada ya muda wa ziada kuanza Chamakh akaifungia Arsenal, bao la tano na kuiweka mbele kwa mara ya kwanza, lakini mshambulizi wa Reading Pavel Pogrebnyak, alijibu dakika chache baadaye na kufanya mambo kuwa 5-5.

Kisha Walcott akafunga lingine na kurejesha Arsenal kileleni kabla ya Chamakh kufunga la saba.

Baada ya kushinda kwa bao moja kwa bila siku ya Jumapili katika mechi yao ya ligi kuu ya Premier ya England na Manchester United, leo Chelsea inapata fursa ya kujaribu kulipisa kisasi kipigo hicho wakati watakapokutana tena katika uwanja wa Stampford Bridge, kwenye mechi ya kuwania kombe la ligi.

Hata hivyo Chelsea itakosa huduma za wachezaji wake nyota, John Terry, Fernando Torres na Branislav Ivanovic ambao wanatumikia adhabu yao baada ya kupigwa marufuku na kupewa kadi nyekundi na Frank Lampard ambaye bado anauguza jeraha.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.