Mkutano kuhusu malengo ya milenia London

Imebadilishwa: 31 Oktoba, 2012 - Saa 10:36 GMT

Njaa ni tatizo kubwa sana barani Afrika

Mkutano unafanyika leo mjini London kujadili mkakati mpya wa utakaotumika baada ya ule wa malengo ya milenia.

Malengo hayo yaliwekwa mwaka elfu mbili kuimarisha maisha ya watu katika nchi maskini na walitumai kuwa yangefikiwa mwishoni mwa mwaka 2015.

Aidha malengo hayo yananuia kukabiliana na maswala kama viwango vya umaskini, magonjwa , njaa na ukosefu wa elimu lakini mafanikio yamekuwa kidogo sana ikilinganishwa na matumaini ambayo watu walikuwa nayo.

Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron, anafanya mazungumzo na Rais Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia na Rais Susilo Bambang Yudhoyono wa Indonesia, wenyekiti watatu wa jopo la umoja wa mataifa litakalopewa jukumu la kuweka mkakati mwingine mwaka 2015 kwa sababu ya malengo ya milenia.

Mwandishi wa BBC anasema kuwa wale wanaohudhuria mkutano wa London watahitaji kutafakari ikiwa swala la malengo ya kupata misaada ni wazo la kizamani liliopitwa na wakti.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.