Mama na mwanawe gerezani Pakistan

Imebadilishwa: 1 Novemba, 2012 - Saa 11:40 GMT

Mraibu wa Heroin

Kesi ya mwanamke muingereza aliyeshtakiwa kwa kujaribu kuingiza kilo 63 za dawa ya kulevya aina ya Heroin nchini Pakistan, imeanza kusikilizwa leo katika mahakama moja mjini Rawalpindi, huku kukiwa na wasiwasi kuhusu mwanawe ambaye yuko gerezani naye.

Mawakili wa Khadija Shah, wanasema kuwa mtoto wake ambaye yuko chini ya miaka miwili,huenda akafa kutokana na hali mbaya magerezani.

Khadija mwenye umri wa miaka 25 alifikishwa mahakamani akimpakata mwanawe, Malaika.

Mama na mtoto wake wanalala ndani ya gereza ambalo limesongamana watu na lenye ulinzi mkali ambako mawakili wake wanasema magonjwa ya ukambi na kifua kikuu yamegundulika.

Maisha ya mtoto huyo yamo hatarini kulingana na shirika la kisheria la Uingereza Reprieve, ambalo linasema mtoto huyo hajapata chanjo, anaharisha sana na kwamba ametibiwa na madawa na kuondoa maumivu ambayo hayafai kwa mtoto mdogo. ''Tunahofia sana kuwa huenda akafariki,'' alisema wakili wa mama huyo Shahzad Akbar.

Khadija Shah alikuwa mja zmito alipokamatwa mwezi Mei akiabiri ndeg kurejea mjini Birmingham.

Maafisa wa Pakistan wanasema alikamatwa na kilo 63 za Heroin ingawa alisema alikuwa anambeba mtu mzigo huo na wala hakujua kilichokuwemo. Ikiwa atapatikana na hatia huenda akanyongwa lakini hukumu hiyo haijatekelezwa nchini humo tangu mwaka 2008.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.