Wanamgambo wavamia bunge la Libya

Imebadilishwa: 2 Novemba, 2012 - Saa 10:59 GMT
Wanamgambo wanaothibiti Bunge la Libya

Wanamgambo wanaothibiti Bunge la Libya

Wanamgambo waliojihami kwa bunduki, wamekalia bunge la Libya, kuelezea masikitiko yao kuhusiana na jinsi serikali mpya ya nchi hiyo ilivyoundwa.

Wanamgambo hao wanataka baadhi ya mawaziri kuondolewa, kwa sababu wanatuhumiwa kuwa na uhusiano na rais wa zamani wa nchi hiyo Muammar Gaddafi.

Malori kadhaa, yakiwa yamesheheni silaha za kutungulia ndege zimejipanga nje ya bunge la nchi hiyo.

Libya iliandaa uchaguzi wa amani mwezi Julai mwaka huu, na wanasiasa wa nchi hiyo waliafikiana kuhusu jinsi ya kubuni serikali mpya siku ya Jumatano.

Waziri Mkuu Ali Zidan alipataa uungwaji mkono kutoka kwa bunge la nchi hiyo kuhusiana na jinsi alivyowachagua mawaziri wake.

Waziri huyo mkuu aliwateuwa wanasiasa wasioegemea upande wowote na wenye misimamo ya kadri, katika baraza lake ili serikali yake ya mseto ikubalike na pande zote.

Lakini mazungumzo hayo yalivurugwa na maandamano mapema wiki hii na siku ya Jumatano, watu waliokuwa wamejihami kwa bunduki, walivamia bunge la nchi hiyo na wamekuwa wakilidhibiti tangu wakati huo.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.