Milingoti ya simu yashambuliwa Nigeria

Imebadilishwa: 4 Novemba, 2012 - Saa 14:54 GMT

Taarifa kutoka Nigeria zinaeleza kuwa kituo cha polisi kimeshambuliwa pamoja na shule ya msingi na milingoti miwili ya simu, katika mji wa Fika, kaskazini-mashariki mwa nchi.

Nigeria

Wakaazi wa mji wanasema mabomu yalirushwa kwenye sehemu hizo leo asubuhi.

Taarifa zisizothibitishwa zinasema askari polisi wawili wamekufa.

Majimbo ya kaskazini mwa Nigeria yameathirika vibaya katika miaka ya karibuni kutokana na ghasia zinazofanywa na kundi la Waislamu la Boko Haram.

Mwezi Septemba kundi hilo lilishambulia zaidi ya milingoti 20 ya simu za mkononi, kaskazini mwa nchi.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.