Mafuriko mabaya zaidi kuwahi kutokea Nigeria

Imebadilishwa: 7 Novemba, 2012 - Saa 03:59 GMT

Mafuriko Nigeria

Zaidi ya watu milioni mbili nchini Nigeria waliathirika kutokana na mafuriko na hivyo kulazimika kutoroka makwao mwaka huu

Idara ya kukabiliana na majanga nchini humo,(Nema) inasema kuwa mvua kubwa zilisababisha vifo vya watu 363 tangu mwezi Julai.

Hayo ndiyo yalikuwa mafuriko mabaya zaidi katika miaka hamsini kuwahi kutokea nchini humo na yameathiri maeneo mengi ya nchi hasa maeneo yaliyo katika mto Niger.

Mwandishi wa BBC nchini Nigeria, Will Ross anasema kuwa maji yameanza kupungua lakini bado kuna hofu ya kupungua kwa chakula kwani wakulima waliharibikiwa na mazao yao mashambani.

Rais Goodluck Jonathan mwezi jana, alitaja mafuriko hayo kama janga la kitaifa lakini alisema kuwa tatizo hilo halitasababisha ukosefu wa chakula.

Duru zinasema kuwa ukosefu wa nyenzo za kuzuia mafuriko ndio tatizo kubwa katika miji mingi ambayo imeshuhudia mafuriko baada ya mvua kubwa.

Katika maeneo mengine ya mashinani watu walielezea hofu ya kuingiliwa na wanyama kama mamba, nyoka na hata viboko ndani ya nyumba zao.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.