Waziri wa zamani UK mashakani kuhusu Rwanda

Imebadilishwa: 8 Novemba, 2012 - Saa 09:41 GMT

Rwanda imekuwa ikidaiwa kuunga mkono waasi wa M23 ingawa imekana

Waziri wa zamani ya usatawi wa kimataifa nchini Uingereza, Andrew Mitchell, anatarajiwa kufika mbele ya kamati ya bunge kueleza kwa nini alitoa ufadhili wa dola milioni 20 kwa Rwanda katika siku yake ya mwisho ofisini.

Msaada huo ulikuwa umezuiwa na Uingereza kufuatia madai ya Rwanda kuunga mkono makundi ya waasi katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Hata hivyo, bwana Mitchell alibatilisha uamuzi wa serikali kutoipa Rwanda msaada.

Rwanda inakana madai ya kuunga mkono waasi, lakini wahisani wengine ikiwemo Muungano wa Ulaya na Marekani zimeendelea kusitisha msaada.

Waziri huyo wa zamani, alilazimishwa kujiuzulu baada ya kuwatukana maafisa wa polisi nje ya makao ya waziri mkuu.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.