Akamatwa na sehemu za siri za mpwa wake A. Kusini

Imebadilishwa: 9 Novemba, 2012 - Saa 07:33 GMT

Ramani ya Afrika Kusini

Mwanamume mmoja nchini Afrika Kusini amekamatwa baada ya kupatikana akiwa na sehemu za siri kwenye pochi lake ambazo zinaaminika kuwa za mpwa wake ambaye hajulikani aliko.

Msemaji wa polisi, aliambia BBC kuwa babada ya kukamatwa kwake , mwanaume huyo aliwapeleka maafisa wa polisi kwenye msitu katika mkoa wa Eastern Cape, ambako mwili uliokatwakatwa ulipatikana.

Kichwa cha msichana huyo pamoja na miguu yake ilikuwa imekatwa na zilipatikana karibu na kiwiliwili chake.

Mtu huyo mwenye umri wa miaka 42, anatarajiwa kufikishwa mahakamani kwa kosa la mauaji.

Mmwanaume huyo alishtakiwa baada ya kushukiwa kuhusika na kutoweka kwa msichana huyo mwenye umri wa miaka 18, aliyepotoea katika mji wa Ngcobo siku ya Jumapili.

Msemaji wa polisi, Mzukisi Fatyela alisema kuwa sehemu hizo za siri, zilipatikana ndani ya pochi lake.

Alisema sababu ya kuuawa kwa msichana huyo haijulikani na kwamba uchunguzi unafanyika.

Alipoulizwa ikiwa mauaji hayo yanahusishwa na waganga ambapo sehemu za mwili wa watu hutumiwa kwenye madawa yao, bwana Fatyela alisema kuwa hawezi kubaini hilo kwa sasa.

Kumekuwa na visa vingi vya kuuza sehemu za siri za watu katika sehemu nyingi za Afrika kwa sababu sawa na hizo.

Afrika Mashariki imeshuhudia visa vingi vya kuuawa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi au maalbino, huku sehemu za miili yao zikikatwa kwa sababu za kishirikina.

Mwanaume huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.