Afungwa miaka 40 A. Kusini kwa pembe za vifaru

Imebadilishwa: 9 Novemba, 2012 - Saa 14:44 GMT

Vifaru wanakabiliwa na tisho la kuwindwa kiharamu

Mahakama nchini Afrika Kusini imemhukumu kifungo cha miaka arobaini raia mmoja wa Thailand aliyepatikana na hatia ya kuuza pembe za vifaru na kuandaa maonyesho ya uwindaji yasiyokubalika

Chumlong Lemtongthai alikiri kosa la kuwalipa makahaba kuweza kufanya maonyesho ya uwindaji wa vifaru.

Pembe hizo ziliuzwa barani Asia ambako soko la pembe hizi ni kubwa sana kwani hutumiwa kama dawa.

Zaidi ya vifaru miatano wameuawa nchini humo na wawindaji haramu mwaka huu pekee.

Akitoa hukumu hiyo jaji alisema kuwa hataki wajukuu wake wakuwe bila kujionea vifaru nchii humo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.