Pakistan yatunza wapatao elimu ya msingi

Imebadilishwa: 10 Novemba, 2012 - Saa 12:26 GMT

Rais Asif Ali Zardari wa Pakistan amesema serikali yake itaanzisha sera mpya ya kuhimiza watoto zaidi kwenda shule.

Malala Yousafzai

Familia maskini kabisa za Pakistan zitapewa fedha ikiwa watoto wao wanakwenda shule ya msingi.

Tangazo hilo limetolewa wakati Pakistan inatimiza mwezi mmoja tangu msichana wa shule wa miaka 15, Malala Yousafzai, kupigwa risasi kaskazini-magharibi mwa nchi.

Malala alishambuliwa na Taliban baada ya kuonekana anatetea elimu ya wasichana.

Kisa hicho kiliwashtua wananchi wengi pamoja na ulimwengu.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.