Soko kuu la punda lafungwa Nigeria

Imebadilishwa: 13 Novemba, 2012 - Saa 11:29 GMT

Nyama ya punda huliwa nchini Nigeria

Muuzaji mkubwa katika soko kubwa la punda nchini Nigeria ametekwa nyara na watu waliokuwa wamejihami.

Polisi wanasema kuwa kutekwa nyara kwa Al-Haji Salisu Yunusa,kumesababisha kufungwa kwa soko hilo ambalo lilijengwa miaka themanini imepita,mjini Ezamgbo.

Mwandishi wa BBC anasema kuwa watekaji hao wanaaminika kutaka kikombozi ili kumwachilia mfanyabiashara huyo.

Takriban punda 200 huchinjwa kila siku katika soko hilo kwa matumizi ya watu.

Kwa mujibu wa msemaji wa polisi Sylvester Igbo anasema kuwa juhudi zimeshika kasi kumtafuta bwana Yunusa.

Mwandishi wa BBC Abdussalam Ibrahim Ahmed, mjini Enugu, anasema kuwa anaelewa watekaji wanataka dola milioni moja nukta 9 kama kikombozi kabla ya kumwachilia mfanyabiashara huyo.

Hata hivyo kuna wasiwasi kuwa bwana Yunusa,anayetoka Kaskazini mwa Nigeria, huenda alilengea kufuatia mauaji ya watu wa Kusini katika eneo hilo.

Soko hilo lilifungwa siku ya Jumatatu huku wauzaji wakiandamana kupinga kutekwa kwake.

Hata hivyo lilifunguliwa baadaye huku wauzaji wakihofia kuwa kufungwa kwake kungezua hali ya wasiwasi na kutatiza harakati za kuweza kuokolewa kwa bwana Yunusa.

Uuzaji na ununuzi wa punda na nyama ya punda kumenawiri kama biashara katika soko hilo tangu kufunguliwa kwake miaka themanini iliyopita.

Takriban malori 20 ya punda huletwa katika soko hilo, kila siku.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.