Xi athibitisha kiongozi mpya wa Uchina

Imebadilishwa: 15 Novemba, 2012 - Saa 09:49 GMT
Viongozi wapya wa Uchina

Viongozi wapya wa Uchina

Xi Jinping amethibitishwa rasmi kuwa mtu ambaye ataiongoza Uchina katika kipindi cha miaka kumi ijayo.

Bwana Xi, aliongoza mkutano wa kamati kuu ya chama cha Kikomunisti nchini Uchina maarufu kama Politburo uliofanyika katika ukumbi wa baraja la mji mkuu wa nchi hiyo Beijing, hatua inayoashiria kupandishwa kwake kuwa kiongozi wa chama hicho tawala.

Akiongea wakati wa mkutano huo Bwana Xi alisema kuwa, chama hicho kinakabiliwa na changamoto nyingi lakini atafanya kazi ili kuhakikisha kuwa ameafikia matakwa na matarajio ya raia wa nchi hiyo.

Wengi wa viongozi wapya katika kamati hiyo wanaonekana kuwa wanasiasa wahafidina na wale waliokisiwa huenda wakaleta mabadiliko hawakupandishwa cheo.

Xi Jinping anachukua mahala pa Hu Jintao, ambaye chini ya utawala wake, uchumi wa Uchina umekuwa kwa kiasi kikubwa.

Hatua hiyo sasa imekalisha shughuli rasmi ya kukabithi madaraka ya nchi kwa kizazi kipya.

Baada ya mkutano huo kukamilika, Bwana Xi, aliondoka kwenye ukumbi huo akifuatwa na Bwana Li Keqiang, ambaye atamrithi Waziri mkuu wa nchi hiyo Wen Jiabao, na wanachama wengine watano wenye ushawishi mkubwa katika kamati hiyo kuu ya chama, ambayo awali ilikuwa na wanachama Tisa lakini imepunguzwa hadi wanachama Saba.

Watano hao ni pamoja na makama wa rais, Zhang Dejiang, kiongozi wa chama hicho mjini Shangai, Yu Zhengsheng, afisa mkuu anayehusika na masuala ya habari na propaganda Liu Yushan, Naibu Waziri Mkuu
Wang Qishan na kiongozi wa chama cha Tianjin Zhang Gaoli.

Viongozi hao wana majukumu makubwa na Bwana Xi, amesema dhamira yao kuu ni kuunganisha na kuongoza chama hicho na kuifanya taifa hilo kuwa thabiti na lenye ushawishi zaidi.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.