Cisse matatani

Imebadilishwa: 15 Novemba, 2012 - Saa 18:22 GMT
Papiss Cisse

Papiss Cisse

Kocha wa klabu ya Newcastle Alan Pardew amesema Papiss Cisse huenda akakosa mechi yao ya jumamosi dhidi ya swansea kutokana na mzozo na timu ya taifa ya Senegal.
Mchezaji huyo ambaye alitarajiwa kujumuika na kikosi cha taifa cha senegal hiyo jana wakati wa mechi yao ya kirafiki alijiondoa kutokana na kile alichokitaja kama jeraha la mgongo.

Senegal imeripotiwa kutisha kutumia sheria ya fifa ya kumpiga marufuku mchezaji huyo kutocheza mechi tano zijazo ikiwa haitapokea ripoti kamili kuhusu hali ya afya ya mchezaji huyo.

Cisse, 27, ameifungia Newcastle mabao matatu msimu huu.

Newcastle imeshinda mechi moja kati ya mechi sita zilizocheza la ligi kuu msimu huu.

Na kutokuwepo kwake katika mechi hiyo ya Jumamosi dhidi ya Swansea ambayo imo alama moja nyuma yao itakuwa pigo kubwa kwa klabu hiyo.

Pardew amesisitiza kuwa wasimamizi wa shirikisho la mchezo wa soka nchini Senegal walifahamishwa kuhusiana na jeraha la Cisse, ambalo alilipata wakati wa mechi yao siku ya Jumapili wakati walilazwa kwa bao moja kwa bila na West Ham.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.