Suluhu baina ya Israel na Gaza yatafutwa

Imebadilishwa: 18 Novemba, 2012 - Saa 16:41 GMT
Waziri wa Mashauri ya nChi za Nje wa Israel, Avigdor Lieberman

Mjini Cairo juhudi za kutafuta makubaliano ya kusitisha mapigano baina ya Israel na Wapalestina wa Gaza zimezidishwa.

Ujumbe wa Israel umewasili Cairo na kwenda moja kwa moja kwenye mazungumzo na wakuu wa Misri.

Jumamosi Misri ilifanya mazungumzo na wakuu wa Hamas, waziri mkuu wa Uturuki na mfalme wa Qatar.

Waziri wa Mashauri ya nchi za Nje wa Israel, Avigdor Lieberman, alisema shuruti ya kwanza na ya lazima kabla ya kusitisha mapigano, ni kwamba Wapalestina lazima waache kurusha makombora kutoka Gaza kuyaelekeza Israel.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.